Kuna aina tatu za mbegu za vitunguu maji zinazotumiwa sana hapa tanzania na wakulima nazo ni kama ifuatavyo .
1. MBEGU ZA KIENYEJI:
Hizi ni zile mbegu zinazozalishwa na wakulima wenyewe. Mara nyingi mbegu hizi zinakua hazijathibitishwa na wataalamu kutoka taasisi ya kuthibiti ubora wa mbegu (TOSCI). Wakulima wanazalisha mbegu hizi na kuwauzia wakulima wengine kwa kutumia kipimo cha kilo au debe.
Wakulima wengi hupendelea mbegu hizi za kienyeji kwa vile bei yake ni ndogo. Mbegu hizi maeneo mengi huuzwa kati ya 20,000 hadi 30,000 kwa Kilo moja ya mebgu. Kutokana na kwamba mbegu hizi zina ubora mdogo, mkulima inambidi atumie mbegu nyingi ili kutosheleza mahitaji ya ekari moja. Kwa ekari moja mkulima hutumia kilo 6 hadi 10 za mbegu hizi ili kutosheleza. Kama mtaalamu wa kilimo simshauri mkulima anayetaka kulima kibiashara kutumia mbegu hizi za kienyeji kwa maana hata Mavuno yake hayatabiriki.
Ila Sio kwamba mbegu zote zinazozalishwa na wakulima ni mbaya, hapana. Upo utaratibu wa wakulima kuzalisha mbegu kitaalamu kwa kufuata utaratibu ulipo kisheria. Mbegu hizo zinazozalishwa na wakulima kitaalamu huitwa mbegu za daraja la kuazimiwa (quality declared seeds) au kwa kifupi huitwa QDS. Mbegu hizi za QDS zina mipaka yake ya eneo la kutumika. Na wazalishaji wa QDS lazima wapate mafunzo na wasajiliwe na Taasisi ya Uthibiti Ubora wa Mbegu (Tanzania Official Seed Certification Institute) au kwa kifupi TOSCI. TOSCI pia wana utaratibu wa kufanya ukaguzi na kutoa kibali cha mbegu hizo za QDS kuuzwa kama zimekizi vigezo husika. Kama hazijakizi mbegu hizo haziruhusiwi kuuzwa kwa wakulima.
2. MBEGU ZA KAWAIDA (OPEN POLLINATED VARIETIES)
au kwa kifupi huitwa OPV. Mbegu hizi zimezalishwa kitaalamu kwa njia ya Uchavushaji ya wazi (Open Pollination). Mbegu hizi ndio zinazouzwa kwa wingi na makampuni ya mbegu. Bei yake ni kati ya 60,000 hadi 100,000 kwa kilo. Hii inategemeana na kampuni na aina ya mbegu. Mbegu hizi kwa ekari moja utatumia Kilo 3 hadi 4. Mfano wa mbegu za OPV ni: Bombay Red, Red Creole, Tajirika, Meru Super n.k.
3. MBEGU CHOTARA (HYBRID):
Hizi ni aina ya mbegu zinazozalishwa kitaalamu sana kuliko hizo aina nyingine nilizozitaja hapo juu. Mbegu hizi hua na sifa za kipekee, kama vile kua na mavuno mengi, kuwa na ukinzani kwa baadhi ya magonjwa, kukomaa haraka n.k. Nyingine hutengenezwa kutokana na sifa maalumu zinazohitajika na walaji au soko, kama vile rangi, ukubwa (size), harufu, ladha n.k. Pia mbegu hizi huuzwa ghali zaidi. Bei yake ni kati ya 300,000 hadi 600,000 kwa Kilo moja. Kilo moja na nusu au Kilo 2 hutosha kwa ekari moja. Mfano wa mbegu hizi ni kama Neptune F1, RedStar F1, JAMBAR F1 n.k
UKIITAJI KITABU CHA KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI NA SWAUMU WASILIANA NASI 0782723170 AU 0743512580
HARDCOPY SH 10,000
SOFTCOPY SH 5,000 UNATUMIWA KWA EMAIL AU WHATSAPP
No comments:
Post a Comment