Showing posts with label VIAZI. Show all posts
Showing posts with label VIAZI. Show all posts

19/08/2021

KILIMO CHA VIAZI MVIRINGO - SEHEMU YA PILI - MBEGU BORA ZA VIAZI MVIRINGO

 

Hili jambo la muhimu sana kwa mkulima kutambua ni aina gani ya mbegu anatakiwa kupanda na ina patikana wapi. Pia ni muhimu kujua hata ni ukubwa gani wa mbegu za viazi unafaa kutumika kupanda. Wakulima baadhi hupanda mbegu za viazi zilizo katwa vipande vipande, na wengine hutumia kiazi kizima lakini vidongo.

Kitaalam inashauri mbegu ya viazi iliyosahihi kwa kupandwa haitakiwi kukatwa vipande vipande, hali hii husababisha mwanya wa wadudu na magonjwa kuingia na kushambulia mbegu mara baada ya kupanda. Mbegu inatakiwa kuwa nzima, na yenye ukubwa wa saizi ya yai la kuku (28-35milimita).


 

SIFA ZA MBEGU BORA ZA VIAZI

Ø  Zenye kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja

Ø  ziwe zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi zaidi ya manne

Ø  zisiwe na wadudu pamoja na magonjwa

Ø  zitoke katika aina ambayo haishambuliwi na magonjwa kama vile ukungu na mnyauko

Ø  zenye ukubwa wa wastani unaolingana na ukubwa wa yai la kuku

AINA ZA VIAZI

Viazi mviringo vipo aina mbalimbali zilizoingizwa    Afrika Mashariki kutoka Ulaya ambako huzalishwa kwa wingi.Kuna aina nyingi sana ya viazi mviringo lakini hapa nitataja aina ambazo nazifahamu na ni bora kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo uyole

Ø   baraka

Ø   sasamua

Ø   tana

Ø   subira(EAI 2329)

Ø   Bulongwa

Ø   kikondo(CIP 720050)

lakini pia kuna aina nyingine nyingi za kigeni ambazo zinafanya vizuri sana katika mazingira yetu ya kitanzania ambazo ni kama vile

1.                 DUTCH ROBIJN – KUTOKA HOLLAND

inavumilia kidogo ugonjwa wa ukungu – hushambuliwa sana na Mnyauko Bakteria – hupendwa na walaji wengi.

2.                 ROSLIN – KUTOKA SCOTLLAND

Ø  ngozi yake ni nyeupe

Ø  ndani ni nyeupe

Ø  huvumulia ugonjwa wa ukungu.

Ø  Kerr’s Pink –

Ø  ngozi yake ni nyeupe au nyekundu

Ø  ndani ni nyeupe

Ø  hushambuliwa sana na ukungu na Mnyauko Bakteria.

3.                 ATZIMBA – KUTOKA MEXICO

– huvumilia ugonjwa wa ukungu

JINSI YA KUANDAA MBEGU BORA YA VIAZI MVIRINGO

Wakulima wengi wamezoea kuandaa mbegu zao za viazi kwa kuchambua mbegu hizo mara tu baada ya kuvuna. Uchambuzi hufanyika kwa kuangalia zile ndogondogo na kuzihifadhi kwa ajili ya msimu unaofuata. Pia kuna wakulima wengine ambao hutegemea kupata au kununua mbegu kutoka kwa wakulima wengine walio jirani au kwenda sehemu fulani kununua mbegu za viazi.

Hali hii kitaalam haishauriwi, kwani kununua mbegu kwa mkulima bila kujua usalama wa mbegu hizo, ni hatari sana, kwani hupelekea mkulima kuuziwa mbegu zenye magonjwa au wadudu. Kwa kufanya hivyo pia huweza kuambukiza magonjwa na wadudu kutoka shamba moja na linguine.

Mkulima anashauriwa kununua mbegu bora kutoka kwa wakulima waliosajiliwa kwa ajili ya kuzalisha mbegu, na kuziuza kwa wakulima wa viazi vya chakula. Vile vile mkulima anaweza kununua mbegu kutoka kwa makampuni yanayojishughulisha na uzalishaji wa mbegu za viazi mviringo.

 

UKIITAJI KITABU CHA KILIMO CHA VIAZI WASILIANA NASI 0782 723170 AU 0743512580 

 

HARDCOPY SH 10,000

SOFTCOPY SH 5,000 UNATUMIWA KWA EMAIL AU WHATSAPP 

KILIMO CHA VIAZI MVIRINGO - SEHEMU YA KWANZA

 

UTANGULIZI

Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zinazoendelea. viazi husitawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita 1300 hadi 2700 juu ya usawa wa bahari. hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano. viazi mviringo vina virutubisho vingi mfano vitamin, protin,madini na maji

Viazi mviringo au Viazi Ulaya ni zao ambalo lina asili ya zao mzizi (tuberous crop) na linalodumu, kwa jina la kitalaam linaitwa Solanum tuberosum.

Neno “Kiazi” linatokana na maana ya mmea ambao una aina “tuber” yaani chenyewe. Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zinazoendelea. Viazi hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano. Viazi mviringo vina virutubisho vingi mfano vitamin, protin,madini na maji.

ASILI YAKE

Viazi mviringo kwa mara ya kwanza viligundulika huko kusini mwa nchi ya Peru na kufuatiwa kaskazini magharibi mwa nchi ya Bolivia kati ya miaka 8000 na 5000 kabla Yesu hajazaliwa (BC). Na vimekuwa viki sambaa kwa kasi katika maeneo tofauti duniani na kuwa zao la chakula katika nchi nyingi.

Hapa Tanzania viazi mviringo kuzalizwa katika maeneo yenye miinuko ya kaskazini kama vile Arusha, Moshi, Lushoto na meneo ya kusini yenye miinuko kama vile Njombe mkoani Iringa na wilaya za mkoa wa Mbeya na mkoa wa Songwe. Pia maeneo ya Morogoro yenye miiunuko hususani Tarafa ya Mgeta yameonekana kuweza kuzalisha zao hili kwa wingi.

 

 

 

 

UMUHIMU WA VIAZI MVIRINGO/ MATUMIZI:

Viazi mviringo vina asilimia kubwa ya chakula chenye asili ya wanga. Viini kama vile vya protini, madini, vitamini na maji. Hivi vyote hutosheleza mahitaji ya mwili wa binadamu.

Pia viazi mviringo hutumika kama zao la biashara kuweza kumpatia mkulima ffedhaza kujikimu na mahitaji mengineyo katika familia.Ili mkulima aweze kulima na kuzalisha kwa tija mbegu bora na kupata mavuno mengi, ni lazima afuate kanuni bora za uzalishaji wa zao la viazi.

Mambo ambayo mkulima anatakiwa kufahami ni pamoja na:

1.          Hali ya hewa kwa zao la viazi ü Hali na aina ya udongo ü Virutubisho ndani ya udongo ü Magonjwa na wadudu ü Namna ya kuvuna na kuhifadhi mbegu na viazi vya chakula.

2.          Ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mbegu na viazi vya chakula.

Kijitabu hiki kinaelezea kanuni bora za uzalishaji wa zao la viazi mviringo. Mkulima anashauriwa kukisoma kwa makini, ili aweze kujua kwa undani

HALI YA HEWA INAYOFAA KILIMO CHA VIAZI

Ili viazi ziweze kumea na kustawi, vinahitaji mazingira na hali ya hewa nzuri inayoruhusu viazi kustawi. Kimsingi viazi zinahitaji hali ya ubaridi na miinuko ya kuanzia erefu wa mita 800 mpaka 3000 kutoka usawa wa bahari. Hata hivyo kwa wakulima wa mbegu, wanatakiwa kuwa na mashamba ya mbegu sehemu zenye miinuko ya juu, ili kuepuka na milipuko ya magonjwa yanayo weza kushambulia na kuharibu mbegu za viazi.

Viazi vinahitaji joto la wastani kuanzia 10-220C. Pia viazi vinahitaji angalau masaa 12 ya mwanga ili viweze kustawi vizuri shambani na kuleta mavuno yenye tija. Udongo unaofaa unatakiwa uwe wenye tindikali ndogo kuanzia 5.0-5.5, hivyo mkulima anashauriwa kufanya uchunguzi wa hali ya tindikali ya udongo kabla ya kupanda. Tindikali ya udongo ikizidi kiwango cha kitaalam, husababisha mazao kushindwa kupata virutubisho kutoka kwenye udongo.

UKIITAJI KITABU CHA KILIMO CHA VIAZI WASILIANA NASI 0782 723170 AU 0743512580 

 

HARDCOPY SH 10,000

SOFTCOPY SH 5,000 UNATUMIWA KWA EMAIL AU WHATSAPP