Hili jambo la muhimu sana kwa mkulima kutambua ni aina gani ya mbegu anatakiwa kupanda na ina patikana wapi. Pia ni muhimu kujua hata ni ukubwa gani wa mbegu za viazi unafaa kutumika kupanda. Wakulima baadhi hupanda mbegu za viazi zilizo katwa vipande vipande, na wengine hutumia kiazi kizima lakini vidongo.
Kitaalam inashauri mbegu ya viazi iliyosahihi kwa kupandwa haitakiwi kukatwa vipande vipande, hali hii husababisha mwanya wa wadudu na magonjwa kuingia na kushambulia mbegu mara baada ya kupanda. Mbegu inatakiwa kuwa nzima, na yenye ukubwa wa saizi ya yai la kuku (28-35milimita).
SIFA ZA MBEGU BORA ZA VIAZI
Ø Zenye kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja
Ø ziwe zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi zaidi ya manne
Ø zisiwe na wadudu pamoja na magonjwa
Ø zitoke katika aina ambayo haishambuliwi na magonjwa kama vile ukungu na mnyauko
Ø zenye ukubwa wa wastani unaolingana na ukubwa wa yai la kuku
AINA ZA VIAZI
Viazi mviringo vipo aina mbalimbali zilizoingizwa Afrika Mashariki kutoka Ulaya ambako huzalishwa kwa wingi.Kuna aina nyingi sana ya viazi mviringo lakini hapa nitataja aina ambazo nazifahamu na ni bora kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo uyole
Ø baraka
Ø sasamua
Ø tana
Ø subira(EAI 2329)
Ø Bulongwa
Ø kikondo(CIP 720050)
lakini pia kuna aina nyingine nyingi za kigeni ambazo zinafanya vizuri sana katika mazingira yetu ya kitanzania ambazo ni kama vile
1. DUTCH ROBIJN – KUTOKA HOLLAND
inavumilia kidogo ugonjwa wa ukungu – hushambuliwa sana na Mnyauko Bakteria – hupendwa na walaji wengi.
2. ROSLIN – KUTOKA SCOTLLAND
Ø ngozi yake ni nyeupe
Ø ndani ni nyeupe
Ø huvumulia ugonjwa wa ukungu.
Ø Kerr’s Pink –
Ø ngozi yake ni nyeupe au nyekundu
Ø ndani ni nyeupe
Ø hushambuliwa sana na ukungu na Mnyauko Bakteria.
3. ATZIMBA – KUTOKA MEXICO
– huvumilia ugonjwa wa ukungu
JINSI YA KUANDAA MBEGU BORA YA VIAZI MVIRINGO
Wakulima wengi wamezoea kuandaa mbegu zao za viazi kwa kuchambua mbegu hizo mara tu baada ya kuvuna. Uchambuzi hufanyika kwa kuangalia zile ndogondogo na kuzihifadhi kwa ajili ya msimu unaofuata. Pia kuna wakulima wengine ambao hutegemea kupata au kununua mbegu kutoka kwa wakulima wengine walio jirani au kwenda sehemu fulani kununua mbegu za viazi.
Hali hii kitaalam haishauriwi, kwani kununua mbegu kwa mkulima bila kujua usalama wa mbegu hizo, ni hatari sana, kwani hupelekea mkulima kuuziwa mbegu zenye magonjwa au wadudu. Kwa kufanya hivyo pia huweza kuambukiza magonjwa na wadudu kutoka shamba moja na linguine.
Mkulima anashauriwa kununua mbegu bora kutoka kwa wakulima waliosajiliwa kwa ajili ya kuzalisha mbegu, na kuziuza kwa wakulima wa viazi vya chakula. Vile vile mkulima anaweza kununua mbegu kutoka kwa makampuni yanayojishughulisha na uzalishaji wa mbegu za viazi mviringo.
UKIITAJI KITABU CHA KILIMO CHA VIAZI WASILIANA NASI 0782 723170 AU 0743512580
HARDCOPY SH 10,000
SOFTCOPY SH 5,000 UNATUMIWA KWA EMAIL AU WHATSAPP
No comments:
Post a Comment