19/08/2021

KILIMO CHA UYOGA - SEHEMU YA KWANZA

 

UTANGULIZI

Je, unataka kustawisha uyoga? Zipo sababu nyingi za kutaka kufanya hivyo. Uyoga ni zao zuri la biashara; uyoga ni rahisi kidogo kusitawishwa, na una protini nyingi sana, vitamin B na madini. Vi l e vile uyoga una kemikali za matibabu. Muda kati ya kupanda na kuvuna ni wiki tatu na mfupi. Zaidi ya hayo, baada ya kuvuna, mkatetaka ni mbolea.

Kitabu hiki kinakupa maelezo kamili juu ya ustawishaji wa uyoga aina ya oyster. Ingawa zipo aina nyingi za uyoga zinazostawishwa, tumechagua zile ambazo zinaweza kustawishwa katika nchi zinazoendelea kwa kutumia teknolojia rahisi.

Unapochagua njia yako ya kustawisha uyoga, budi ujiulize na kujibu maswali yafuatayo:

1 Ni aina ipi ya uyoga unayotaka kustawisha?

2 Chunguza soko (wanunuzi) na pia joto muafaka kwa aina hiyo ya uyoga.  

3 Je, unaweza kupata mbegu ya uyoga wa aina unayotaka  kustawisha?

4 Ni aina gani ya mkatetaka unayohitaji ili kuweza kustawisha aina ya uyoga unaohitaji?  

5 Je, utatunza vipi mkatetaka? Hii inahusiana na uwekezaji mtaji ulio nao.

Kwa kuelewa ustawishaji uyoga, pamoja na sifa za uyoga budi ujue elimu juu ya elimuviumbe ihusuyo uyoga. Kwa hiyo tutaanza na elimuviumbe ya uyoga.

Uyoga ni aina ya nyuzi kuvu yenye kutofautiana na mimea mingine kwa kukosa chembe chembe zinazowezesha mimea kujitengenezea chakula yenyewe kwa kutumia hewa na mwanga.

Uyoga unaota wenyewe kwenye mashamba hasa wakati wa mvua kwenye maeneo yenye mboji nyingi. Sasa hivi nchini tunao utaalamu wa kuotesha uyoga au ndani ya nyumba au nje kwenye kivuli maalumu.

Uyoga umefahamika na wanadamu tangu enzi za zamani sana. Miaka elfu nne kabla ya kuzaliwa Kristo watu walijua uyoga. Historia inatueleza kwamba watu wameanza kulima kwa utaalamu mwaka 300 baada ya kuzaliwa Kristo.

Wadadisi wa mambo wanauelezea Uyoga kufanana sana na chakula waisraeli walichokuwa wakila kule jangwani katika safari yao ya kutoka utumwani Misri.

Wakati Uyoga ukilimwa katika dunia yote, hapa Afrika na hasa kwetu Tanzania mambo yalikuwa ni tofauti kabisa. Hakuna mtu aliyesumbuka na kilimo hicho. Ni hapo majuzi tu mwaka 1993 ndipo ukulima ulianza Dar es salaam. Mwaka 1994 ukulima ulianza Arusha, mwaka 1995 ukulima ulianza  Mbeya, na mwaka 2003 ukulima ulianza huko Kilimanjaro.

Miaka ya karibuni, utaalamu wa kuotesha uyoga umeanza hapa Tanzania baada ya watu kutilia maanani lishe bora ya protini na manufaa mengine ya zao hilo. Kwa kuwa uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za kuoteshea, urahisi wa teknologia ya kuotesha katika mazingira ya Tanzania na soko lake kwa wananchi na katika hotel. Hata hivyo ni wananchi wachache tu wanaojua kilimo cha uyoga.

Aina zinazofaa kwa Tanzania ni zile ambazo hustawi vizuri, kwenye maeneo ya joto la wastani wa nyuzi joto 20C hadi 33C. Kwa mfano uyoga aina ya mamama n.k. Aina hizi za uyoga pia uhitaji hali ya unyevu hewani (moisture) wa kiasi cha asilimia 75%.

Uyoga ni chakula kizuri sana na chenye virutubisho vingi vinavyohijika katika mwili wa mwanadamu, Wataalumu wengi wa afya na tiba wanautumia katika kutibu magonjwa mbalimbali kwa mwanadamu, Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa uyoga unavitamini za kutosha pamoja na protini.

FAIDA ZA UYOGA

Ø    Uyoga una maajabu makubwa katika maisha ya mwanadamu, Uyoga ni lishe bora kwa mwanadamu , ni dawa na tiba kwa mwanadamu, ni zao la kuingizia watu kipato, ni rafiki wa mazingira pia.

Ø    Lishe kama protini inayolingana na ile ipatikanayo kwenye maziwa, samaki na kunde. Pia utapata vitamini B, C, na D, na madini ya joto, phosphoras, chuma na potashi.

Ø    Uyoga husadikika kutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, moyo, shinikizo la damu na figo.

Ø    Masalia ya mazao hutumika katika kuzalishia uyoga, na baada ya kilimo cha uyoga yanaweza kutumika kama mbolea asili kwa kilimo cha bustani. Masalia ya kilimo cha uyoga pia hutumika kama chakula cha mifugo kama ng’ombe.

Ø    Kilimo hiki huhitaji eneo dogo sana la ardhi na kiasi kidogo cha maji, hivyo hupunguza tatizo la ukosefu wa ardhi na ugomvi katika jamii ambao unatokana na tatizo hilo.

Ø    Kilimo hiki ni cha mwaka mzima, na mzunguko wa kwanza ni kati ya wiki 6 mpaka 12

Ø    Kilimo hiki ni njia nyepesi ya kutoaajira kwa familia kutokana na gharama ndogo, teknolojia rahisi inayotumika na pato lake kubwa.Calcium na Potash.

LISHE

Ø    . Uyoga ni zao lenye viini lishe (amino acids) zote 22 zinazohitajika na mwili wa mwanadamu.

Ø    . Protini iliyoko kwenye Uyoga inafikia kiwango cha asilimia arobaini. Hii inalingana na protini iliyoko kwenye maziwa.

Ø    . Kuna wingi mkubwa sana wa vitamini B,C na D.

Ø    . Uyoga hauna mafuta mengi. Una asilimia tatu tu. Hivyo hauna Colestrol.

 

UKIITAJI KITABU CHA KILIMO BORA CHA UYOGA WASILIANA NASI 0782723170 AU 0743512580 

HARDCOPY SH 10,000

SOFTCOPY SH 5,000 UNATUMIWA KWA EMAIL AU WHATSAPP 

No comments:

Post a Comment