UTANGULIZI
Vitunguu maji kwa kitaalamu hujulikana kama Allium cepana kwa kiingereza huitwa Bulb Onions. Vitunguu ni zao muhimu sana sio kwa matumizi ya ndani tu lakini pia ni zao la kibiashara linaloweza kukuletea kipato kikubwa. Vitunguu ni zao la bustani ambalo lipo kwenye kundi la mboga (vegetables). Zao hili ni maarufu kutokana na thamani ya virutubisho ilivyonavyo na ladha yake kwenye mapishi ya vyakula mbalimbali.
Vitunguu ni zao la pili ambalo hutumika karibu kila siku katika mlo wa familia za kitanzania. Afrika Mashariki, na Dunia Nzima. Vitunguu vina chukua nafasi kubwa katika matumizi ya mboga hasa kwa wakazi wa mijini. Vitunguu hutumika katika kutengeneza kachumbari, kiungo cha mboga, nyama na samaki. Majani ya kitunguu hutumika kama mboga. Vitunguu pia hutumika kutengeneza supu n.k
Nchini mwetu vitunguu hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Tanga, Arusha sehemu za Mang’ora na Babati, Kilimanjaro, Singida, Morogoro, Iringa wilaya ya Kilolo mpakani mwa mkoa wa Morogoro na kwenye maeneo ya mto Ruaha , Mara , Morogoro wilayani Kilosa sehemu za Lumuma na Malolo , Mbeya Kilimanjaro na baadhi ya sehemu za Mkoa wa Singida. Katika shamba lililo hudumiwa vizuri na kupandwa katika hali ya hewa na aina ya mbengu. Vitunguu hutoa kiasi cha tani (10) hadi 16 kwa ekari moja.
Kilimo cha Vitunguu ni mojawepo ya vilimo vyenye manufaa mengi kwa ajili ya matumizi ya kila siku ya vitunguu kwa maisha ya mwanadamu, kiafya, kitabibu na kwa ajili ya kutengeneneza au kuchanganyia katika dawa tofauti. Pia ni kiungo mahususi katika mambo ya mapishi.
Hapo awali kitungu kilikuwa ni zao lililokuwa linapatikana porini katika ukanda wa bahari ya Mediterania. Zao hili hulimwa katika nchi nyingi za magharibi, nchi za milima zilipo kaskazini mwa dunia, likwemo bara la Afrika. Vitunguu hustawi katika hali ya hewa ya jotoridi 13°C – 24°C, hali ya hewa inayofaa kwa kuotesha na kukuzia miche kwenye kitalu ni jotoridi 20°C – 25°C. Kwa kawaida vitunguu huhitaji kiasi cha joto nyuzi 20°C-25°C ili kuweza kustawi na kukua vizuri. Joto zaidi ya hapo hufanya vitunguu kudumaa na kutoweza kutengeneza viazi (bulbs).
AINA ZA VITUNGUU MAJI
Kuna aina nyingi ya vitunguu maji. Aina hizi zinaweza kutofautishwa kulingana na:
(i) rangi ya ganda la nje la kitunguu kilichoishavunwa;
(ii) radha (utamu au ukali) wa kitunguu chenyewe; mahitaji ya mwanga katika uzaaji: kuna aina yenye kuhitaji siku fupi (mwanga wa saa 10 hadi 12 kwa siku) na aina ihitajio siku ndefu (saa 13 hadi 14 za mwanga kwa siku) ili kuweza kuweka kitunguu. Aina ya kwanza ndiyo ilimwayo katika nchi za tropic.Vitunguu maji vimegawanyika katika makundi matatu:
1. VITUNGUU VYEUPE (WHITE ONIONS).
Vitunguu hivi ni vyeupe nje na ndani pia: Mfano ni White granex, snow white
2. VITUNGUU VYA NJANO (YELLOW ONIONS).
Vitunguu hivi hua na rangi ya dhahabu kwa nje, ila ndani nyama yake ni ya njano mpauko. Vitunguu hivi ni vitamu (ladha ya sukari) kuliko aina nyingine ya vitunguu. Mfano: Texas Supersweet, Walla Walla Sweet, Granex Yellow Hybrid, Candy Hybrid
3. VITUNGUU VYEKUNDU (RED ONIONS):
Hivi vina rangi nyekundu kwa nje na ndani kunakua na rangi nyeupe. Mfano Red Creole, Red Bombay, Neptune F1, Tajirika, Meru Super, Mangâ Red, JAMBAR F1, n.k
Aina hizi za vitunguu vyekundu ndizo hupendwa zaidi na walaji na ndio huzalishwa kwa wingi. Hivyo katika mafunzo yetu tutajikita zaidi kwenye aina hizi za vitunguu vyekundu.
UKIITAJI KITABU CHA KILIMO CHA KITUNGUU MAJI NA SWAUMU WASILIANA NASI 0743512580 AU 0782723170
HARDCOPY SH 10,000
SOFTCOPY SH 5,000 UNATUMIWA KWA EMAIL AU WHATSAPP
No comments:
Post a Comment